April 30, 2008

Austria kunani?

Fritz F.

Wakati waandishi wa habari kutoka duniani kote wanafika kwa wengi katika mji mdogo wa Amstetten nchini Austria, polisi imeendelea kuchunguza nyumba ya familia ya mzee Josef Fritzl kutafuta ushahidi mwingine. Wengi wanajiuliza vipi mzee huyu mwenye umri wa miaka 73 aliweza kumficha binti yake Elisabeth kwa muda huu mrefu wa miaka 24 pamoja na watoto wao katika chumba cha chini ya ardhi bila ya wengine kujua. Kwa muda huu wote alimbaka Elisabeth.
Polisi leo imechunguza ikiwa mlango wa chumba hiko uliweza kuwekwa na mtu mmoja bila ya msaada. Mlango huu una uzito wa kilogram 300 ulio wa chuma cha pua na mazege na wenye ufunguo wa elektroniki na unafunguliwa kwa kutia nambari ya siri. Mkuu wa upepelezi wa makosa ya jinai nchini Austria, Franz Polzer, alikanusha kwamba mzee Fritzl alikuwa na wasaidizi.
Bw. Joseph Fritzl alianza kumbaka binti yake Elisabeth alipokuwa na umri wa miaka 11. Wakati mtoto alifika umri wa miaka 18, baba yake alimtega kwenye chumba cha chini ya ardhi na kumficha huko. Tangu hapo hakuwa tena na dalili yeyeto kuhusu binti huyo. Katika muda huu wa miaka 24 katika gereza lake, Elisabeth alizaa watoto saba, baba yake akiwa pia baba wa watoto hao. Mtoto mmoja alikufa, wengine watatu mzee aliwapeleka juu kwenye nyumba na kumwambia mke wake kwamba Elisabeth aliwaacha mlangoni. Mbele ya familia yake, mzee huyu alisema, binti yake Elisabeth alikimbia nje ya Austria kuishi na kundi la kidini. Watoto wengine watatu waliishi na mama yao katika chumba cha chini ya ardhi.
Kulingana na mkuu wa polisi ya mji, Bw. Heinz Lenze, hakuna aliyejua kuhusu maisha ya wafungwa hao. Afisa alisema: “Aliunda picha kamili kabisa na mtuhumiwa alikuwa mwenye madaraka katika familia yake. Kulingana na uchunguzi wetu, si mke wala familia waliojua kuhusu maovu ya mzee huyo.”
Hata maafisa wa idara za serikali waliochunguza nyumba nzima miaka 9 iliyopita hawakugunda maficho chini ya ardhi. Utekaji huu mzima uligunduliwa baada ya mfungwa Elisabeth aliweza kuzungumza na polisi baada ya kumsindikiza mtoto mmoja hospitalini. Polisi ilisema hali ya binti huyu ni mbaya sana, anaonekana kuwa miaka 20 mzee kuliko umri wake.
Kwenye picha zilizochapishwa na polisi unaweza kuona sehemu fulani ya maficho yaliyokuwa na jiko, choo na bafu pamoja na vyumba viwili vya kulala. Kwa ujumla maficho haya yalikuwa na ukubwa wa mita 60 za mraba.
Majirani wa familia hiyo bado wanashindwa kuelezea yaliyoendelea. Mmoja alieleza kuhusu namna, mzee aliweza kununua vyakula: “Alikwenda madukani kwa gari, lakini alikwenda hadi miji mingine, kwa hivyo haikujulikana kwamba ananunua vyakula vingi hivi.”
Kwa wakati huu, polisi pia inachunguza kesi nyingine ya mauaji na ikiwa mzee Fritzl alihusika naye. Pia kuna tuhuma nyingine ya ubakaji dhidi ya mzee huyu. Polisi inafikiria sasa kuwapa wahanga wa familia hiyo majina mapya.


Elisabeth ambaye alifungiwa na baba yake chini ya nyumba

Habari kutoka kwa marafiki zake wa karibu zinasemekana yakuwa mzee huyu alikuwa akimfungia mwanaye na watoto (wajukuu ?) katika chumba hicho chenye dirisha moja tu na yeye kwenda likizoni Thailand bila kuwa na huruma na binadamu hao ambao amewafanya kama wafungwa wake. iwapo mzee huyo atapatikana na hatia katika kesi ambayo imeanza kusikilizwa
jana katika mahakama moja huko Amstetten Austria basi anasubiriwa na kifungo cha maisha.
Mzee huyo inasemekana kutokuonyesha hata huruma kutokakana na kitendo hicho cha kinyama alichokifanya.
mambo kama haya yangetokea katika nchi moja wapo ya Africa yangezungumzwa kila kona ya nchi zilozoendelea na kushirikishwa na mambo ya uzembe na ushirikina, sasa kitu cha kushangaza ni kwamba miaka yote hiyo 24 katika nchi kama hii ambayo inavifaa vya kila aina katika mambo ya uchunguzi walishindwa kweli kugundua kama kuna watu wamefungiwa chini ya nyumba? nia aibu kubwa sana na uzembe wa polisi.

No comments: