April 29, 2008

Chumba kidogo

Mtuhumiwa Josef Fritz.

Hii ndio sehemu aliyofungiwa Elizabeth kwa kipindi cha miaka 24


Mzee anayetuhumiwa kumfungia kwenye chumba bintiye na kisha kuzaa naye watoto saba anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo huko Austria.
Mzee huyo Josef Fritz mwenye umri wa miaka 73 hapo jana alikiri kuwa alimfungia mwanaye huyo wa kike aitwaye Elizabeth kwa kipindi cha miaka 24 ambapo alizaa naye watoto saba.
Mkuu wa upepelezi wa makosa ya Jinai nchini Austria Franz Polzer alisema mmoja wa watoto hao saba aliyozaa na mwanaye alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa na kwamba aliutelekeza mwili wa kichanga hicho kwenye tanuri la nyumba yao.

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Dunani kuna mambo!:-(

Chemi Che-Mponda said...

Kuna watu ambao tunawaon ni wazima kabisa. Kumbe ndo wehu. Halafu kuna watu ambao tunasema ni wehu kumbe ni wazima. Kweli duniani kuna mambo!