April 15, 2008

Ndege yaanguka katika eneo linaloishi watu mashariki ya Goma.

Maafisa wa serikali nchini jamhuri ya kidemokrasi ya Congo wamesema kuwa ndege chapa DC-9 imeanguka katika eneo la nyumba zinazoishi watu katika mji wa mashariki mwa Congo wa Goma.
gavana wa jimbo la Kivu ya mashariki Julien Mpaluku amesema kuwa ndege hiyo ilipata matatizo wakati ikianza kuruka na kuangukia katika eneo linaloishi watu wengi.
Kundi la waokoaji liko njiani kwenda kwenye eneo la ajali. Idadi ya watu waliouwawa hadi sasa imefikia watu 78.
Hata hivyo kamanda wa jeshi linalolinda eneo la uwanja wa ndege wa Goma , Gauthier Iloko, amesema kuwa watu kumi hadi sasa wameokolewa kutoka katika mabaki ya eneo la ajali wakiwa hai.
Ndege hiyo imeanguka leo katika kitongoji cha Birere, ambacho kiko karibu na uwanja wa ndege. Ndege hiyo ilikuwa inatoka mjini Goma kwenda Kisangani.
Ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya binafsi ya Hewa Bora.

No comments: