April 28, 2008

UBAKAJI AUSTRIA

Polisi wakiwa katika nyumba ya Mtuhumiwa

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 73 amekiri kuzaa na mtoto wake wa kike watoto saba, baada ya kumfungia mtoto wake huyo kwenye chumba kisicho na dirisha chini ya nyumba yake kwa muda wa miaka 24.
Mzee huyoJosef Fritzl ambaye ni fundi wa umeme mstaafu kutoka Kusini mwa Austria alikiri kumfungia mwanaye huyo wa kike aitwaye Elisabeth kwenye chumba hicho toka mwaka 1984.
Elizabeth ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 42 aliambia polisi kuwa baba yake huyo miaka 24 iliyopita alimshawishi kwenda naye kwenye chumba kilichoko chini ya nyumba yao ambako alimlewesha na kumfunga pingu na kumfungia.
Mwanamke huyo ambaye alitoweka toka mwaka 1984 alipatikana Jumamosi iliyopita, baada ya polisi kudokezwa kuwepo kwake kwenye chumba hicho.
Amesema kuwa baba yake huyo alianza kufanya naye mapenzi toka alipokuwa na umri wa miaka 11.

No comments: