MANENO MACHAFU NA KASHFA HAZINA NAFASI KATIKA KIWANJA HIKI. TUNAKARIBISHA MAONI YENYE KUJENGA NA KUELIMISHA JAMII.
June 22, 2008
KAMBI YA MISS TANZANIA EU KUANZA JUMATATU
Kambi ya washiriki wa kumtafuta mrembo wa kitanzania katika nchi za Schengen yaani miss tanzania Schengen,inatarajiwa kuanza jumatatu hii ambapo vimwana 10 kutoka nchi mbalimbali za jumuiya yaUlaya watashiriki.Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika jumamosi ijayo katika ukumbi wa EFES mjini Essen Ujerumani ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mh Ahmada Ngemera.Mratibu wa shindano ambalo kwa mara ya kwanza linafanyika katika nchi za Schengen, Nashe Mvungi amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwa pamoja na kuongezeka kwa wadhamini.Amesema kuwa wadhamini hao ni Gazeti la African Positive lililoko Dortmund nchini Ujerumani ambalo pia linamiliki magazeti mengine maarufu kwa jamii yawaafrika barani Ulaya http://www.africa-positive.de/ ,wadhamini wengine Ethiopian airline kutoka Frankfurt , African Heritage na African Courier,http://www.africaonline24.com/ .Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bi Veve Tata amesema magazeti hayo yataingia mkataba na mrembo atakayeshinda ili kumtafutia mikataba ya urembo katika nchi nyingine hapa barani Ulaya.Wadhamini wengine wa shindano hilo ni shirikala ndege la Ethiopea airline pamoja na kampuni ya utalii ya Western Tours ya Bonn Ujerumani.Katika shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau kutoka nchi mbalimbali za ulaya msanii wa kizazi kipya kutoka Tanzania anayetamba na kibao chake Cinderela Ali Kiba atatumbuiza, pamoja na msanii kutoka Cameroon wa miondoko ya Makossa Eyum Anneh.Tiketi za onyesho hilo zimekuwa zikiuzwa kwa kasi katika vituo mbalimbali.Bei ya tiketi hizo ni euro 10,lakini kwa wale watakaonunua mlangoni ni euro 15 pamoja na kinywaji kimoja bure.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22
-
NDUGU,JAMAA, MARAFIKI NA WADAU WA BLOG HII YA JAMII NASIKITIKA KUWATAARIFU YA KUWA NIMEPATWA NA MSIBA WA MAMA YETU MPENDWA BI KHADIJA( NA...
-
blog hii bado inatengenezwa na unakaribishwa kwa maoni. Pia unakaribishwa kuangalia website yetu mpya http://kilimanjarostars.de/ .
No comments:
Post a Comment