Viongozi wa kampuni ya magari ya Marekani General Motors pamoja na maafisa wa utawala wa nchi hiyo wamekamilisha mipango ya kuwasilisha ombi la kusaidiwa kampuni hiyo isifilisike na pia isaidiwe kufanya mageuzi. Kampuni ya General Motors inatarajiwa kuwasilisha ombi kwa mujibu wa ibara ya 11 ya sheria ya muflis hii leo mjini New York Marekani kabla masoko ya fedha kufunguliwa.
Duru zilizo karibu na kamati ya wenye dhamana zinasema wawekezaji wamekubaliana kuhusu mpango unaowapa asilimia 25 ya umilikaji wa kampuni ya General Motors itakayofanyiwa mageuzi.
Mpango huo ambapo serikali ya Marekani itamiliki asilimia 70 ya hisa za kampuni ya General Motors kwa mabadilishano ya mkopo wa dola bilioni 60, unaelezwa kuwa mkubwa kuwahi kutokea nchini Marekani kuhusu muflis katika viwanda.
No comments:
Post a Comment