August 26, 2011

KIKONGWE ALALA NA MAITI SIKU 6 AKIDAI ALIKUWA HAJUI LOLOTE, ARIPOTI

MAANDALIZI YA MAZISHI
MASHUHUDA WA TUKIO HILO KATIKA MTAA WA ILOLOMAANDALIZI YA KUUZIKA MWILI WA MAREHEMU
MWILI WA MAREHEMU UKITOLEWA
SHEIKH AKIMWOMBEA DUA MAREHEMU
MAITI IKISWALIWA

Yasemekena aliwahi kumuua mkewe na kufungwa jela miaka 8
· * Wanakijiji wamtaka ahame, Polisi yaingilia kati

KIKONGWE mwenye umri wa miaka 85 aliyefahamika kwa jina la Sadiki Salehe mkazi wa Ilolo kata ya Ruanda Jijini Mbeya amejikuta matatani kufuatia kulala na maiti ya mtoto wake pekee kwa siku sita.

Habari za kuaminika kutoka kijijini hapo zimesema kuwa wakati harufu hiyo ikiendelea kuzagaa eneo la nyumba yake na majirani, Kikongwe huyo alikuwa akiendelea kuandaa futari karibu na mlango wa chumba cha marehemu hasa ukizingatia huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mtoto wa kikongwe huyo alijulikana kwa jina la Salehe Sadiki(38) kwa mara ya mwisho alionekana Jumatano ya wiki liliopita(Agosti 17, 2011).

Kikongwe huyo alipohojiwa alisema kuwa Jumatano ya Agosti 24 mwaka huu akiwa nyumbani kwake alikuwa anahitaji dishi la kuogea ambalo lilikuwa katika chumba cha marehemu ambaye alikuwa akiishi nje ya nyumba ambayo ilikuwa ikitizama na ya baba yake umbali wa meta 1.5.
Na mara baada ya kuchukua hatua ya kutaka dishi hilo ndipo alipoenda na kugonga mlango wa chumba cha marehemu na kukuta mlango ukiwa umefungwa huku harufu ikitoka kwa mbali.

Harufu hiyo ilimshtua kikongwe huyo ambaye aliamua kwenda msikiti wa Soweto uliopo Jijini Mbeya kwa Imamu Eliasa Selemani ambaye naye alimtaarifu balozi wa mtaa huo Iddi Malole kuhusu tukio hilo.

Imamu Eliasa na Balozi Malole kwa pamoja walimtaarifu Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Benson Mbwana kuhusu tukio hilo la kushangaza ambaye alimua kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Mwanjelwa.

Kituo cha Polisi cha Mwanjelwa kilishindwa kushughulikia suala hilo ambalo lilipelekwa katika kituo cha Polisi cha Kati (CENTRAL POLICE) ambacho kiliruhusu kuzikwa kwa mwili huo ambao ulikuwa umeharibika vibaya kwa kupasuka huku Polisi ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Wakati Polisi wakitoa amri ya kuzikwa kwa mwili huo wakazi wa mtaa huo walipandwa na hasira kufuatia tukio hilo na walisikika wakisema kuwa sio mara ya kwanza kwa mzee huyo ambaye hapo awali alimuua mkewe na kumweka uvunguni mwa kitanda kwa zaidi ya siku nne hali iliyomfanya atumikie kifungo cha zaidi ya miaka 8 jela kutokana sakata hilo.

Polisi walipoona hayo ilimuondoa mzee huyo eneo la tukio kwa nguvu ili kunusuru maisha yake.

Wakati polisi ikiondoka na mzee huyo wakazi hao walisikika wakisema mzee huyu hatakiwi kurudi tena kijijini hapo kutokana na vitendo hivyo licha ya sura yake ya upole aliyonayo na kushinda msikitini.

Aidha Mwenyekiti wa mtaa huo alisema sula hilo sasa limo mikononi mwa Jeshi la Polisi hivyo watalishughulikia ipasavyo.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22